Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhwan Jakaya Kikwete , Agosti 27 2025, Dar es Salam amekutana kwa mazungumzo na Mhe. Gembá Koichiro, Makamu Spika wa Baraza la Wawakilishi la Japan yaliyolenga kuimarisha uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Japan kwenye sekta za maendeleo ya rasilimali watu hususan hasa vijana.