Mgombea Urais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT Wazalendo Ndg.
Luhaga Mpina akiambatana na Mgombea Mwenza Ndg. Fatma Ferej, leo 08
Agosti 2025 wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Chama na kupokelewa na
Kiongozi wa Chama Ndg. Dorothy Semu
Viongozi wengine
waliowapokea wagombea hao ni pamoja na Makamu Mwenyekiti Bara Ndg.
Isihaka Mchinjita Katibu Mkuu Ndg. Ado Shaibu, KC Mstaafu Ndg. Zitto
Kabwe Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama Ndg. Mhonga Ruhwanya
pamoja na Maafisa mbalimbali wa Chama Makao Makuu.