Mgombea wa nafasi ya Udiwani katika Kata ya Ilala kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Saady Kimji, leo Agosti 18, 2025, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea kupitia chama chake. Hatua hiyo ni sehemu ya mchakato wa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Kimji aliwashukuru maafisa wa tume kwa mapokezi mazuri na uratibu wa zoezi hilo huku akihaidi kufanya kampeni za kistaraabu kupia chama hiko.
"Zoezi la kwanza la uchukuaji wa fomu nimelikamilisha. Kinachofuata ni kurudisha fomu ili kupata ridhaa rasmi ya kugombea udiwani kupitia CCM. Ninawahakikishia INEC kuwa kampeni zetu zitazingatia misingi ya uhuru na amani," alisema Kimji.Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa Kata ya Ilala ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa kata hiyo, Bi. Vumilia Ng’wavi, aliwakumbusha wagombea wote umuhimu wa kujaza fomu kwa umakini na kufuata maadili ya uchaguzi katika kipindi chote cha kampeni.
Hata hivyo Kimji anawania nafasi hiyo kwa mara ya pili, akilenga kuwakilisha wananchi wa Ilala kwa ufanisi zaidi kupitia ilani na sera za chama cha Mapinduzi CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo.