Chama cha ACT-Wazalendo kimekamilisha safu yake ya juu ya wagombea wa nafasi ya urais kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumteua Ndugu Fatma Abdulhabib Ferej kuwa Mgombea Mwenza wa urais wa Luhaga Mpina ambaye amechaguliwa kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Uteuzi huo umetangazwa rasmi wakati wa Mkutano Mkuu wa chama hicho, ambapo wajumbe walipitisha jina la Ferej kwa kauli moja kufuatia mapendekezo ya Kamati Kuu ya chama.