Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Elie Mpanzu ,siku ya leo amejiunga na wachezaji wenzake kambini Ismailia nchini Misri tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26 wa ligi kuu ya Tanzania bara pamoja na michuano ya Kimataifa barani Afrika (CAF).
Mpanzu amejiunga na timu moja kwa moja kutoka nchini kwao Congo Drc alipokuwa mapumzikoni huku sababu ya kuchelewa kujiunga na timu ikitajwa ni kutokukamilika kwa vibali vya kuingia nchini Misri ambavyo baada ya kukamilika aliweza kusafiri na kujiunga na timu siku ya leo.
Tags
Michezo