Chama cha ACT
Wazalendo kinatarajia kufanya Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa siku ya
Jumatano, tarehe 06 Agosti, 2025, katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini
Dar es Salaam.
Mkutano huu utafanyika kwa mujibu wa Ibara ya 61
ya Katiba ya ACT Wazalendo ya Mwaka 2015, Toleo la mwaka 2024, ambayo
inatoa mamlaka ya kuitisha Mkutano Mkuu kwa ajili ya maamuzi muhimu ya
chama.Kabla ya Mkutano Mkuu, kutafanyika vikao vya Kamati Kuu na
Halmashauri Kuu ya Taifa, ambavyo vitafanyika siku ya Jumanne, tarehe
05 Agosti, 2025, katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo Makao Makuu
ya Chama.
Mkutano huo Maalum umeitishwa kwa lengo kuu la kufanya
uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, na Zanzibar, kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.