Kiungo Moussa
Balla Conte leo ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa Klabu ya
Yanga SC, akitokea CS Sfaxien ya Tunisia, baada ya kusaini mkataba wa
miaka mitatu wa kuwatumikia Wananchi.
Awali, usajili wa Conte
uliibua sintofahamu kubwa, huku ripoti mbalimbali za vyombo vya habari
zikimhusisha na Simba SC, ambapo ilidaiwa alikuwa karibu kutua Msimbazi.
Hata hivyo, Yanga SC imeibuka kidedea katika vita ya kumsajili kiungo
huyo, baada ya kumtambulisha rasmi na kuthibitisha kuwa huduma ya kiungo
huyo sasa ni mali ya Wananchi kuelekea msimu mpya wa mashindano.
0 Comments