Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umewekeza maeneo salama
yenye kuuwezesha kupata faida kubwa ikiwemo hati fungani na dhamana za
Serikali na kwa mwaka wa fedha uliomalizika wamepata faida ya trilioni
1.3.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi
PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo kwenye banda la Mfuko huo kwenye Maonesho
ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye
viwanja vya Julius Nyerere, maarufu Sabasaba Julai 7, 2025.
Amesema
asilimia 84 ya uwekezaji uliofanywa na mfuko huo umewekwa maeneo hayo
ya hati fungani ambako kuna uhakika unaoouwezesha Mfuko kupata faida
kubwa na kulipa wastaafu na wanachama wake mafao mazuri na endelevu.
“Tumewekeza
maeneo salama maeneo ambayo yanaleta faida kubwa kwa wakati ili tuweze
kulipa mafao bora kwa wastaafu wetu na wanachama, ndiyo maana asilimia
84 ya uwekezaji wetu tumeuwekeza kwenye amana za serikali na hati
fungani,” alisema Bw. Magambo.
Ameongeza kuwa “Tunapokea
wafanyakazi wapya kila siku na wengine wanastaafu kwa hiyo wakistaafu
wanapaswa wakutane na pensheni yao, ili iwe hivyo lazima tuwekeze fedha
zao kwenye maeneo sahihi yenye faida ya haraka na ya uhakika na
uwekezaji huu unafuata miongozo ya Benki Kuu ya Tanzania BoT,” alisema
Pia
amewahakikishia wanachama wa PSSSF wakiwemo wastaafu kuwa Mfuko uko
salama una ukwasi wa kutosha kuhakikisha mafao yanalipwa kwa wakati siku
zote.
Aidha Kagaruki alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa
kuweka mazingira mazuri ya biashara ambayo yamesababisha jengo hilo refu
zaidi kupata wateja kwa asilimia 80.