Mkuu wa
Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva ameendelea na ziara ya kikazi ya kata
kwa kata katika kuwafikia wananchi wa wilaya hiyo kwa ukaribu na
kutimiza adhma mbalimbali kwa mujibu wa ratiba yake ikiwa ni pamoja na
Kuwa na mkakati maalum wa kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za
wananchi pamoja na Muendelezo wa ukaguzi wa utendaji wa watendaji wa
serikali na kukagua, kuweka mawe ya msingi, kutembelea na kuzindua
miradi mbalimbali iliotekelezwa chini yake Serikali ya awamu ya sita.
Aidha,
Mhe Victoria ameendelea na ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambapo
amepata nafasi ya kufanya ukaguzi wa umaliziaji wa Ujenzi wa mabweni
mawili katika shule ya Sekondari Nangaru- yenye thamani ya 103,727,096
na kuweka jiwe la msingi katika mradi huo sambamba na kuzungumza na
watumishi, wanafunzi na wananchi waishio eneo jirani.
Akiendelea
na ziara yake, Sambamba na hapo DC Mwanziva amekagua Ujenzi wa madarasa 3
na matundu 6 ya vyoo shule ya Msingi Makumba ambapo pia ameweka jiwe la
msingi katika mradi huu wenye gharama ya 83,200,000 na kupokelewa kwa
kishinda na wanachi wenye hamasa kubwa baada ya kupokea mradi huo.
Katika
hatua nyingine, Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika maeneo ya
Mradi DC Mwanziva amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo makubwa ambayo
wana-Lindi wanaendelea kupata na kunufaika katika nyanja na Sekta
mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya, Miundombinu na Kilimo.