Balozi wa
Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, amemuandikia barua Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, akitangaza
kujiuzulu nafasi ya uwakilishi wa Tanzania nchini Cuba, eneo la Karibe,
Amerika ya Kati pamoja na nchi rafiki za Colombia, Venezuela na Guyana
Katika
barua hiyo, Polepole ameeleza kuwa ameamua kujiuzulu kutokana na
mwelekeo wa kiuongozi unaokosa msimamo thabiti katika kusimamia haki za
watu, amani, na heshima kwa wananchi
Aidha, ameeleza
kutoridhishwa na kufifia kwa dhamira ya kweli ya uwajibikaji na
kushughulikia changamoto za wananchi, sambamba na kudorora kwa maadili
ya uongozi
Amesisitiza hawezi kuendelea kuwa sehemu ya uongozi
usiohamasika na utii wa misingi ya katiba ya nchi na chama, haki,
maadili, utu na uwajibikaji kwa wananchi
Polepole aliwahi kuwa
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Novemba 2020 – Machi
2022), Balozi Malawi (Machi 2022 – Aprili 2023) na Cuba (Aprili 2023 –
Julai 2025).