Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 12,2025 amemaliza
mgogoro wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Manzese na Halmashauri ya Ubungo
ambao umetokana na wafanyabiasha hao kushindwa kulipa Ushuru wa Huduma
"Service Levy" ambao ulipelekea wafanyabiasha hao kufunga maduka 11
wakidai Serikali iwatoze ushuru huo kwa "flat rate"

RC Chalamila
amesema Serikali chini ya uongozi mahiri wa Dkt Samia Suluhu Hassan
inawathamini wafanyabiasha na siku zote Rais ameendelea kuweka
mazingira rafiki ya kufanya biashara, hivyo kwa kuwa Ushuru wa Huduma
uko kisheria ni vigumu kubadili takwa hilo la kisheria kwa sasa ni
lazima wizara husika ihusishwe hivyo ni mchakato.
Kwa mantiki
hiyo RC Chalamila amewataka wafanyabiasha hao kuandika maelezo ya kuomba
kupewa muda maalum wa kukamilisha deni hilo ili timu ya watalaam wa
biashara ikae ione namna bora ya wafanyabiasha hao tena mmoja mmoja
atakavyoweza kulipa deni hilo bila kuathiri biashara yake.
Aidha
RC Chalamila amekemea tabia ya uanaharakati kwenye biashara, "migomo
haina tija kamwe usidanganyike kuwa katika vikundi kugoma, biashara ni
ya mtu mmoja mmoja na sio kikundi " Alisema RC Chalamila.