Jabir Mohamed Chilumba kada wa CCM ambaye ni Mkuu wa Idara ya Mipango Manispaa ya Kinondoni, amechukuwa fomu ya kuomba ridhaa ya Wana CCM jimbo la Mtama kupeperusha bendera ya chama hicho kugombea Ubunge wa jimbo hilo, katila uchaguzi utakaofanyika mwezi Oktoba.
Chilumba amewaambia Waandishi wa Habari kuwa uamuzi wake huo ni sahihi na ameufanya kwa muda sahihi akiamini yeye anatosha zaidi, kuwatumikia wana jimbo la Mtama katika zama hizi.
Ameongeza kuwa alitumia muda mrefu kufuatilia changamoto za jimbo hilo na kujiona kuwa haitokuwa busara kwake kuacha kujitokeza kuwa mtatuzi na mfariji wa ndugu zake jimbo la Mtama