Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) linapenda kuuarifu umma kuwa timu ya taifa ya Harambee Stars imejiondoa kwenye Mashindano ya CECAFA Four Nations yanayofanyika nchini Tanzania.
Uamuzi huu umefanyika kufuatia mapendekezo na ushauri kutoka kwa benchi la ufundi la timu, likiongozwa na Kocha Mkuu Benni McCarthy, baada ya tathmini ya kina ya hali iliyopo kwa sasa, ambapo ilionekana kuwa mazingira hayakuwa rafiki kwa ushiriki na maandalizi ya timu kwa ujumla.
Timu itarejea nchini Kenya na kuendelea na maandalizi ya Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024, ambapo sasa mkazo wote utaelekezwa katika kuhakikisha timu inajiandaa ipasavyo kwa majukumu yajayo.
FKF inaendelea kujitolea kuhakikisha timu ya taifa inapatiwa mazingira bora zaidi ya kushindana na kuiwakilisha nchi kwa fahari.
Tags
Michezo