Watumishi
wa Wizara ya Afya wa Makao Makuu ya Wizara leo Julai 21, 2025 wamehamia
rasmi na kuanza rasmi kutoa huduma kwa wananchi katika jengo jipya la
Wizara ya Afya lililopo Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.
Hatua
hiyo inajiri mara baada ya kukamilika kwa jengo hilo ambalo limegharimu
zaidi ya Shilingi Bilioni 26.6 na sasa litawawezesha watumishi wote wa
Wizara ya Afya makao makuu kufanya kazi katika eneo moja, na kuleta
ufanisi na tija zaidi kwa huduma zinazotolewa.
Jengo hilo lina
mita za mraba 14,355 likijumuisha sakafu 10 huku mbili(2) zikiwa ni
sakafu za ardhini (basement), jengo lina ofisi zaidi ya 188 pamoja na
kumbi za mikutano 13.
Wananchi wote wenye uhitaji wa kupata
huduma wakaribishwa kufika katika ofisi hizo mpya muda wa saa za kazi
kuanzia saa moja na nusu asubuhi (07:30 am) mpaka saa tisa na nusu
mchana (03:30 pm) Jumatatu mpaka Ijumaa.
0 Comments