GILEAD TERI ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA UWEKEZAJI NA MAENEO MAALUM NCHINI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (Tanzania Investment and Special Economic Zones Authority -TISEZA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusilika, Bw. Gilead John Teri ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo iliyoanzishwa kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Na. 6 ya Mwaka 2025.

Sheria hiyo imeunganisha majukumu ya kilichokuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na iliyokuwa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (ΕΡΖΑ).

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form