Klabu ya Azam FC imetangaza rasmi kukamilisha usajili wa nyanda Aishi Manula kutoka Simba SC alikodumu kwa miaka minane. Usajili huu umekamilika kwa uhamisho huru, na Manula amesaini mkataba wa miaka miwili hadi mwaka 2027.
Manula mwenye miaka 29 aliondoka Azam FC mwaka 2017 na
kujiunga na Simba SC, ambako alifanikiwa kutwaa mataji mbalimbali ya
ndani na kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara kadhaa.
Hata hivyo, nafasi yake kikosini ilianza kuyumba baada ya kuumia nyonga
mwishoni mwa msimu wa 2022/23, hali iliyomuweka nje kwa miezi sita.
Katika msimu wa 2023/24, alicheza mechi chache tu, huku makipa wengine
kama Ayoub Lakred na Moussa Camara wakipewa nafasi zaidi .
Azam
FC, waliomaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Tanzania msimu
uliopita na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Afrika, wanahitaji uzoefu na
uongozi wa Manula katika safu ya ulinzi. Ujio wake unatarajiwa
kuimarisha kikosi hicho, hasa katika mashindano ya kimataifa na ya ndani
.
Kwa sasa, Manula anatarajiwa kuwa kipa chaguo la kwanza wa
Azam FC kwa msimu wa 2025/2026, akichukua nafasi ya Mohamed Mustafa
ambaye alisumbuliwa na majeraha msimu uliopita.
Kwa mashabiki wa
Azam FC, kurejea kwa Manula ni habari njema na ishara ya dhamira ya
klabu hiyo kutwaa mataji na kufanya vizuri katika mashindano ya
kimataifa.
Tags
Michezo
