Rais Mstaafu
Dkt. Jakaya Mrisho, ameshiriki katika Mkutano Mkuu wa Afrika
ulioandaliwa na Jarida la Uongozi la Afrika (African Leadership
Magazine) na Taasisi ya Uongozi wa Afrika (African Leadership
Organization) jijini London, Uingereza.

Mkutano huo unazungumzia
masuala mbalimbali ya Afrika, ikiwemo Uongozi, Uwekezaji na Ushindani
wa Kimaendeleo kwa kauli mbiu ya: “Powering Leadership, Investment and
Competitiveness”.
Awali, Rais Mstaafu ambaye ni Mwenyekiti wa
Bodi ya Washauri ya African Leadership Organization (ALO), aliongoza
vikao vya Bodi hiyo ambayo inaangazia masuala mbalimbali ya maendeleo ya
Afrika kijamanii na kiuchumi.
Bodi hiyo ina wajumbe kutoka nchi
mbalimbali duniani, akiwemo Dkt. Jewel Howard Taylor, Makamu wa Rais
Mstaafu wa Liberia; Prof. Tahir Akhtar, Mkurugenzi wa Kampuni ya Adam
Global Holdings UK/UAE; Dkt. Victor Oladukon, kutoka Benki ya Maendeleo
Afrika (AfDB); Dkt. Christian Lindfeld, Mwanzilishi na Mkurugenzi
Mtendaji wa Africa Ventures Advisory - Germany; Jenerali William Kip
Ward, Kamanda Mkuu Mstaafu wa Kamandi ya Jeshi la Marekani barani
Afrika; Mhe. Nomvula Makonyane, Makamu Katibu Mkuu wa ANC - Afrika
Kusini; na Dkt. Ken Giami, Mtendaji Mkuu wa African Leadership
Organization (ALO).