Mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaendelea Leo Juni 24, 2025 jijini Dodoma ambapo wabunge watapiga kura kupitisha bajeti kuu ya Serikali ya Tsh. trilioni 56.49 kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Bajeti ambayo inatarajiwa kugharamiwa na mapato ya ndani ya shilingi trilioni 40.47, misaada shilingi trilioni 1.07 na mikopo ya shilingi trilioni 14.95.Kati ya mapato ya ndani yanayotarajiwa, mapato ya kodi ni shilingi trilioni 32.31, mapato yasiyo ya kodi shilingi trilioni 6.48, na mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa shilingi trilioni 1.68.
Aidha, mikopo inajumuisha shilingi trilioni 6.27 kutoka vyanzo vya ndani na shilingi trilioni 8.68 kutoka vyanzo vya nje.
Tags
Habari
