Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro amesema washiriki wa
Maonesho ya 49 Biashara ya Kimataifa (DITF) ili kuzuia uhalifu katika
maonesho hayo kila mtu anapaswa kuwa mlinzi wa mwenzake.

Amesema
kila mmoja anapaswa kuzingatia sheria, miongozo na kanuni zilizoandaliwa
na waandaaji wa maonesho hayo ili kuzuia uhalifu.
Hayo ameyasema siku ya jana Juni 26, 2025
jijini
Dar es Salaam Muliro wakati akitoa mada katika semina ya kuwajengea
uwezo washiriki wa maonesho hayo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo
ya Biashara Tanzania (TanTrade).
"Kila mtu anapaswa kuwa mlinzi
wa mwenzake na kwamba ili ulinzi uweze kufanyika vizuri ni lazima watu
watii sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika maonesho haya,"
amesema.
Kamanda Muliro amesema ni muhimu washiriki wa maonesho
hayo kuepuka kubeba mizigo isiyojulikana au yenye mashaka pamoja na
kuchukua tahadhari vya vitu vyenye asili ya mlipuko.
“Washiriki
wote ni muhimu mkazingatia sheria na kanuni za maonesho, pia mtoe
taarifa haraka kwa walinzi endapo kuna hali ya hatari pamoja na kufuata
miongozo yote ya ulinzi iliyoandaliwa na waandaaji,” amesema
Pia
amesisitiza kuwa hakuna maendeleo yanyaoweza kutokea bila kuwepo kwa
mazingira salama na kwamba ulinzi hutoa msingi wa uwekezaji wa
kibiashara, elimu bora na huduma za afya na miundombinu salama.