TP Mazembe wamekosa rasmi kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.
Sare ya 1-1 na Aigles du Congo leo inawafanya kufikisha pointi 30 katika mechi 16 za mchujo wakiwa nafasi ya 5 kwenye msimamo.
Hilo ni pigo kubwa kwa wababe hao wa Congo na washindi wa medali za fedha za kombe la Dunia la vilabu la FIFA 2010.
Aigles du Congo mabingwa wa Ligi Kuu ndio Wawakilishi wa nchi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tags
Michezo