Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia leo tarehe 07 Septemba 2025. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Pili wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika nchini Ethiopia.