Dkt. Saleh Mohamed Abdallah wa Idara ya Elimu ya Mahakama ya Kadhi, BAKWATA, baada ya wasilisho la Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga Bw. Ramadhani Ndwatah katika Kongamano la Uzinduzi wa Kampeni ya Kurudisha Maadili kwa Jamii kuelekea kumbukizi ya mazazi ya Mtume Mohammed (S.A.W) lililofanyika Wilayani Korogwe.
"Nimefurahi na
nimevutiwa sana na Mada ya Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga, ambayo
imesheheni mafunzo kuhusu Uzuiaji Rushwa na Maadili pamoja na Kongamano
letu la Uzinduzi wa Kampeni ya Kurudisha Maadili kwa Jamii kuelekea
kumbukizi ya mazazi ya Mtume Mohammed (S.A.W).
Ninasisitiza wote tuungane tukatoe mafunzo na kuyaishi maadili yaliyowasilishwa hapa"