Watia nia 11 waliongoza kwenye kura za maoni za Udiwani kupotia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro wameondolewa.
Wakati
zoezi la mchujo katika chama Cha Mapinduzi likiendelea nchini Tanzania
kwa Mkoa Morogoro watia nia 11 waliongoza katika kura za maoni udiwani
kupitia chama hicho wameondolewa kwa kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo
Akitoa
taarifa yake kwa waandishi wa habari ,katibu mkuu wa chama Cha
Mapinduzi (CCM ) Mkoa wa Morogoro ndugu Nuru John Ngereja amesema kuwa
sababu za kutoteuliwa kwa wagombea hao ni pamoja uvunjifu wa
maadili,makundi ndani kwenye kata zao.
Aidha ndugu Ngereja
amezitaja Kata sita ambazo ni Mindu,Mwembesongo,Lukobe,Kilakala,Mbuyuni
na Mlimani kuwa bado zinasubiri maamuzi kutoka kamati maalumu ya Chama
Cha Mapinduzi CCM Manispaa ya mkoa wa Morogoro.
Katibu wa CCM
ndugu Ngereja amesema kuwa wagombea wote walioongoza nafasi ya udiwani
viti maalumu wameteuliwa kwenye nafasi hizo.