Mkurugenzi
Mtendaji wa Manara Tv,Haji Sunday Manara ambaye pia ni Kada Maarufu wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) Manara Leo Julai 01, 2025 amechukua rasmi
fomu ya kuwania Udiwani katika kata ya Kariakoo iliyopo Jimbo la ilala
Jijini Da es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari mara
baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu jumuiya ya wazazi CCM Kata ya
Kariakoo Bi. Shum Gessan, @hajismanara amesema kuwa yeye ni mzaliwa wa Kariakoo na amechukua fomu hiyo kuomba ridhaa ya kuongoza Wananchi wa Kariakoo na viunga vyake.
Haji
Manara ni miongoni mwa makada wakongwe wa Chama cha Mapinduzi na
amewahi kutumikia chama hicho katika ngazi mbalimbali ikiwemo kuwa
Katibu Mwenezi katika Mkoa wa Dar es Salaam.