Timu ya Yanga imethibitisha kuwa Msimu wa Mwaka 2024/25 ni ‘mali yao’, baada ya kutwaa Fainali ya CRDB Bank Federation Cup 2024/2025 kwa kuifunga Singida Black Stars Magoli 2-0 katika Fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan.
Wafungaji waliopeleka furaha kwa Yanga katika mchezo wa leo Juni 29, 2025 ni Duke Abuya dakika ya 40 na Clement Mzize dakika ya 50
Ikumbukwe, Yanga ilianza msimu huu kwa kubeba Ngao ya Jamii, ikashinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya nne mfululizo, na kwa kunogesha zaidi ubingwa huo ilishinda michezo yote miwili dhidi ya Simba ambao ni Wapinzani wao wa Jadi, pia ilitwaa Kombe la Muungano