Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Enock Bella, ameomba radhi hadharani kwa mwimbaji Mbosso kufuatia mahojiano aliyoyafanya mwaka jana ambapo alimuelezea vibaya. Enock Bella amesema kuwa alikosea kama kijana na anatambua kosa lake, hivyo anaomba msamaha kwa Mbosso na kwa Watanzania wote walioumizwa na maneno yake.
"FIRST, kaka yangu na ndugu yangu Mbosso kwanza nichukue nafasi hii kuomba RADHI hadharani kwa kukukwaza kwenye
mahojiano niliyofanya mwaka jana, kama binadamu siwezi kuwa sawa siku
zote na ndio ubinadamu kwa hilo nabeba uwajibikaji na naomba RADHI.
Kama
ulivyosema ROOM NUMBER MOJA ( YAMOTO BAND) ilikuwa si tu band bali
shule nzima ya maisha na viongozi wetu walitufundisha kusaidiana,
kuchukuliana madhaifu, kuwajibika na kuomba radhi ukiteleza, hivyo ndugu
yangu NIWIE RADHI,
Watanzania wapenzi wa Mbosso na Enock Bella nawaomba pia radhi kwa kukwazika sisi bado ni vijana wenu wenye ndoto
za kupambania na supporters wetu ni nyie hivyo kwa lilitokea mniwie
radhi kijana wenu na muendelee kutupa support na tuendelee kuenjoy
miziki mizuri iliyo ndani ya ROOM NUMBER THREE.
Ndugu
zangu wa media naomba sana, sitakuwa na mahojiano tena kuhusu suala
hili kwangu nimelimaliza hapo , ndugu yangu amesema nilichomkwaza na
ninaomba radhi hivyo sina maoni mengine juu ya interview ya kaka yangu Mbosso.
tutafutane kwa maswali mengine ila si kwa swala hili "🙏
Mbosso naye akaja akajibu Hivi,
"Kipindi
Wenzetu Wawili Wametangulia Kupata Management na Kuachia Kazi Zao na
Wakiwa Wanafanya Shows zao .. Mimi na Wewe Ndo Tulikuwa Tunaongea Muda
Mwingi ndani pale Maskani Tabata Savanna…
Niliacha Mziki na Sikuwa
Nataka Mziki Kabisa Baada ya Kuona Ya Moto Band imevunjika .. ila Siku
niliokukuta Unalia Chumbani Peke Yako na Ukasema ‘ Nakunukuu “.. Mbosso
Fanya Mziki Wewe Utanisiadia Naujua Moyo Wako ..” Nilikusikiliza na
niliamua Kuanza Tena Mishe mishe Za Miziki na kwa Baraka Za Mungu Neema
zilianza na nilichagua kushare na wewe Kwenye Kidogo na Kikubwa
nilichopata ..,
Nilifanya Hivyo Kaka Kuanzia Kwenye Shows zangu Hadi
Kwenye Maisha Ya Kawaida Kwa Ujumla … Unajua Kwa Nini …? Kwa Sababu
Kauli Yako Moja ilitosha Sana Kunipa ujasiri na Leo Nipo Hapa …
Love You so Much Bro ❤️🫂
Tags
Burudani