Na Ally Mandai
Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, amesema anaianza michuano ya Kombe la Mapinduzi 2026 akiwa na malengo makuu matatu.
Barker
amesema kwanza anaitumia kuwafahamu vizuri wachezaji, pili ni sehemu ya
kujiandaa na mashindano mengine yanayokuja ikiwamo Ligi ya Mabingwa na
tatu kubeba taji la Mapinduzi.
Simba iliyopo Kundi B, kesho
Januari 3, 2026 itaanza kwa kucheza dhidi ya Muembe Makumbi City kwenye
Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja, kisha Januari 5, 2026 itaikabili
Fufuni, ikiwa mechi ya mwisho hatua ya makundi.
Baada ya michuano
hiyo, Simba ina mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Esperance ya
Tunisia, ikianzia ugenini Januari 23, 2026, kisha nyumbani Januari 30,
2026.
Katika Ligi ya Mabingwa, mechi mbili za kwanza Simba imepoteza, hivyo inaburuza mkia wa kundi D.
0 Comments