Ufaulu wa
matokeo ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne umepanda kwa asilimia
2.67 na asilimia 88 ya wanafunzi wamefaulu na kidato cha pili.

Matokeo
yametangazwa leo Januari 10, 2026 na Katibu Mtendaji wa Baraza la
Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Said Mohamed, mbele ya waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam.
Mtihani wa upimaji wa kidato cha
pili jumla ya wanafunzi 898,718 walisajiliwa wakiwemo wasichana 497,891
sawa na asilimia 55.48 na wavulana 400,827 sawa na asilimia 44.5.
Waliofanya
mtihani huo walikuwa wanafunzi 811,575 sawa na asilimia 91.3 katika
shule za sekondari 6,223. Aidha wanafunzi 77,689 sawa na asilimia 8.7
hawakufanya upimaji huo pamoja na kuwa walisajili.
Jumla ya
wanafunzi 1,583,686 walisajiliwa kufanya mtihani wa upimaji wa darasa la
nne wakiwemo wasichana 818,673 sawa na asilimia 52 na wavulana 765,013
sawa na asilimia 48.
Mahudhurio ya wanafunzi wa darasa la nne
yalikua asilimia 94 sawa na wanafunzi 1,490, 377 katika shule za msingi
20,508 ambapo ufaulu kwa wasichana wamefaulu kwa asilimia 53 huku
wavulana ikiwa asilimia 47.
Aidha, wapo wanafunzi 93,309 sawa na asilimia 6 ambao hawakufanya mtihani huo pamoja na kuwa walisajiliwa.
0 Comments