HIKI NDICHO KIKOSI CHA JESHI LA MAREKANI KILICHOMNG'OA MADARAKANI MADURO

Kikosi cha jeshi la Marekani kilichohusika kumkamata Nicolas Maduro ni cha Delta force ambacho ni kikosi namba mbili kwa uhodari baada ya kile cha juu kabisa cha makomandoo cha Navy Seals kilichomshughulikia Osama Bin Laden

Hawa Delta force ni makomandoo pia ni wazee wa misheni ngumu za kuokoa na kuteka viongozi wakuu wa maadui, wakati Navy Seals ni makomandoo wa misheni ngumu zilizoshindikana na vyombo vyote. Vikosi hivi vina wazee wa kumwaga moto vibaya mno zinapigwa chuma na kwa shabaha za uhakika

Kiufupi Jeshi la Marekani lina vikosi vitatu hatari zaidi na
Vikosi hivyo vitatu hatari zaidi vya jeshi la Marekani vinajulikana kwa uwezo wao wa kipekee, mafunzo ya hali ya juu, na utekelezaji wa operesheni ngumu duniani kote. Vikosi hivyo ni kama ifuatavyo:

1. Navy SEALs (Sea, Air and Land Teams)
- Kikosi cha vikosi vya majini (U.S. Navy).
- Maarufu kwa operesheni ya kumuua Osama bin Laden (2011).
- Hufanya operesheni za siri, uokoaji wa mateka, kupambana na ugaidi, na upelelezi wa kijeshi.

2. Delta Force (1st SFOD-D)
- Kikosi maalum cha siri cha Jeshi la Marekani (U.S. Army).
- Linalenga kukamata au kuuondoa uongozi wa adui, kuokoa mateka, na kupambana na ugaidi.
- Hutambuliwa rasmi kama Special Forces Operational Detachment - Delta (SFOD-D)

3. Marine Raiders (MARSOC – U.S. Marine Corps Forces Special Operations Command)
- Kikosi maalum cha Majini wa Marekani (U.S. Marine Corps).
- Kinashughulika na vita visivyo vya kawaida (unconventional warfare), ujasusi, na operesheni maalum.

Vikosi hivi hufanya kazi kwa kushirikiana na mashirika ya ujasusi (kama CIA) na hutumwa maeneo hatari zaidi duniani.


 

Post a Comment

0 Comments