Na Mwandishi Wetu
TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeaga michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa machungu, baada ya kufungwa kwa bao 1-0 na wenyeji Morocco katika mchezo uliopigwa jana.Bao hilo pekee la mchezo lilifungwa dakika ya 64 baada ya kipa wa Stars, Denis Masalanga, kushindwa kuokoa kwa usahihi shuti hafifu la mshambuliaji wa Morocco, na kuusindikiza mpira wavuni.
Hata hivyo, dakika ya 93, Tanzania ilinyimwa penalti ya wazi baada ya kiungo mshambuliaji Idi Nado kuangushwa ndani ya eneo la hatari, lakini mwamuzi wa mchezo huo alikataa kutoa penalti, licha ya kilio kikubwa kutoka kwa benchi la ufundi la Stars.Kocha wa Taifa Stars, Miguel Gamondi, pamoja na maofisa wa timu hiyo, waliandamana hadi kwa mwamuzi wakimtaka atazame VAR, lakini aliendelea na maamuzi yake na muda mfupi baadaye akapuliza kipenga cha mwisho.
Tanzania sasa inaaga michuano hiyo kwa masikitiko, huku mashabiki na wadau mbalimbali wakilalamikia maamuzi tata yaliyokwamisha juhudi za vijana wa Stars.Taifa Stars yatupwa nje mbele ya Morocco.Timu ya Taifa ‘Stars Stars’ imeondoshwa katika michuano ya Mataifa ya Afrika kwenye hatua ya robo fainali baada kukubali kupigo cha bao 1-0 kutoka kwa Morocco.
Taifa Stars imeaga michuano hiyo ikiandika historia mpya kwa kufuzu hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya Tanzania kufika hatua hii tangu iliposhiriki kwa mara ya kwanza AFCON mwaka 1980.Taifa Stars ilifuzu kama "best loser" baada ya kumaliza nafasi ya tatu katika Kundi C na pointi 2, ikipiku Angola kwa idadi ya mabao ya kufunga. Mechi yao ya mwisho ilikuwa sare ya 1-1 dhidi ya Tunisia, bao la Fei Toto likisawazisha dakika ya 48.



0 Comments