Upinzani mkali na usio na kificho umeibuka ndani ya Kanisa Katoliki baada ya waumini, Mackdeo Shilinde na Gerald Abel, kupinga hadharani kauli walizodai kutolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, wakisema mimbari imegeuzwa jukwaa la matusi, hukumu na vitisho badala ya Injili ya mapendo na umoja.
Katika tamko lao, waumini hao wamesema hawatakubali Kanisa liendeshwe kwa woga na matusi, wakisisitiza kuwa Kanisa si mali ya Askofu wala Padri mmoja, bali ni jumuiya ya waumini.
Matusi Madhabauni Yazua Hasira za Waumini
Kwa mujibu wa waumini hao, Askofu Ruwa’ichi alitumia homilia ya Misa ya Krismasi tarehe 25 Desemba 2025 kuwaita waumini kwa maneno mazito kama “lofa”, “mpumbavu”, “njaa njaa”, “msaliti” na “ndumilakuwili” — kauli walizosema zinakiuka moja kwa moja mafundisho ya Biblia.
Waumini hao wamenukuu wazi Maandiko Matakatifu yanayokataza hukumu na udhalilishaji, wakisema:
“Msihukumu, msije mkahukumiwa.” (Mathayo 7:1)
“Usimhukumu mtumishi wa mtu mwingine.” (Warumi 14:4)
“Neno lenu na liwe daima na neema.” (Wakolosai 4:6)
Kwa mujibu wa waumini, hakuna sehemu ya Biblia inayoruhusu kiongozi wa dini kuwaita waumini wake majina ya kudhalilisha hadharani, hasa kutoka madhabauni.
“Mimbari Imewekwa Kuunganisha, Sio Kuburuzana”
Katika msimamo wao, waumini hao wamesisitiza kuwa mimbari imewekwa kwa ajili ya kuunganisha waumini na kuwafariji, si kuwadhalilisha. Wamenukuu pia:
“Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.” (Mathayo 5:9)
“Jitahidini kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.” (Waefeso 4:3)
Wamesema kauli za matusi kutoka madhabauni zinawakwaza waumini, kinyume na onyo la Biblia linalosema:
“Msiwakwaze wadogo hawa.” (Mathayo 18:6)
Hoja zijibiwe , Waumini Wakaburuzwa
Shilinde na Abel wamesema kauli hizo hazikujibu hata hoja moja kati ya zile zilizowasilishwa kwa mamlaka za juu za Kanisa kupitia barua ya waumini Stanslaus Nyakunga na Elia Phaustine kwa Balozi wa Vatican.
Barua hiyo iliomba tathmini ya mwenendo wa Padri Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), anayelalamikiwa kuhusishwa na siasa za chama kimoja cha CHADEMA.
Kwa mujibu wa waumini, badala ya hoja k7ujibiwa kwa busara au kufanyiwa uchunguzi wa kikanisa, walishuhudia waumini wakiburuzwa hadharani kwa maneno ya dharau.



0 Comments