NA JIMMY CHIKA
KUANZIA mwaka 1989 hadi hii leo wimbo wa bendi ya Tuncut Almas usemao Sina cha kukupa Mama, unaendelea kupamba katika sherehe mbalimbali za kijamii ikiweno harusi.
Umekuwa ni wimbo maarufu unaotumiwa kuelezea hisia za mapenzi kwa akina mama.
Tangu mwaka huo hadi sasa umeendelea kuwa wimbo unaowakilisha mapenzi ya mtoto kwa mama yake.
Mtunzi wa wimbo huu ni marehemu Kasaloo Kyanga ambaye aliwahi kutunga na kuimba nyimbo kama Alimas Super Matimila, Mwanaidi (Orchestra Tomatoma), Karubandika ( Marquiz du Zaire) nk.
Wimbo huo wa Mama aliutunga akiwa na bendi ya Tuncut Alimas, ukirekodiwa Terehe 12.9.89, ambapo gitaa la solo alipiga Kawelee Mutimanwa,
Solo namba 2, Kibambe, Ramadhani, John Kitime, Ridhim William Maselenge na Besi Amani Ngezi.
Wengine walioshiriki ni Akulyake Saleh King Maluu, Abdul Mgatwa, Rey Mlangwa na Buhere Buheti (Trampet).
Juma Tengeneza alipiga Dram na Haruna Lwali aliyezikung'uta Tumba.

0 Comments