Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata madereva watano wa magari ya kubebea wagonjwa kwa tuhuma za kubeba abiria kinyume cha sheria.Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Alex Mkama, amesema madereva hao waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Kagera wamekamatwa kufuatia oparesheni maalum ya kuimarisha usalama barabarani iliyoanza Desemba Mosi mwaka huu. #AzamTVUpdates
0 Comments