SERIKALI KUPUNGUZA GHARAMA ZA UZALISHAJI WA SAMAKI KWA KUJENGA KIWANDA MWANZA

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Ng'wasi Kamani amesema Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi itajenga Kiwanda cha Kutengeneza chakula cha samaki jijini Mwanza kwa lengo la kuwapunguzia gharama wafugaji wa samaki kwa njia ya vizimba jambo litakaloongeza uzalishaji wa samaki nchini.

Kamani amesema hayo wakati akizungumza na wanufaika wa mradi wa vizimba vya kufugia samaki eneo la Kisoko mkoani Mwanza ambapo amesema Wizara hiyo imepanga kujenga kiwanda hicho ili kuwapunguzia mzigo watanzania wenye nia ya kufanya uzalishaji kupitia ufugaji wa samaki.

Ameongeza kuwa Wizara imeshaandaa mpango wa kukutana na wadau wa sekta binafsi ili kuzungumza nao kwa ajili ya kuzalisha vifaranga vya samaki na vyakula vya samaki vitavyopatikana kwa gharama nafuu kwa manufaa ya wananchi.

Aidha, amesema serikali wizara hiyo ipo katika hatua za kuongeza wigo wa mikopo inayotoleea na serikali ili iguse watu wote wanaohusika na mnyororo wa thamani wa sekta uvuvi.
 

Post a Comment

0 Comments