TAIFA STARS YAVUNA BIL.1.9 KWA KUTINGA 16 BORA AFCON
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imejihakikishia kitita cha Dola 800,000 (sawa na Sh. 1,980,252,800) baada ya kutinga hatua ya mtoano wa timu 16 bora kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2025.Stars ilifuzu hatua hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Tunisia kwenye mchezo wa mwisho wa kundi C na hivyo kufuzu kama timu bora iliyoshika nafasi ya tatu.
Mshindi wa AFCON 2025 atapata zawadi ya fedha taslimu dola milioni 10, huku mshindi wa pili atapata dola milioni 4.Hili ni ongezeko kubwa kutoka mwaka 2023, ambapo mabingwa wa mwaka huo, Ivory Coast alipata dola milioni 7 na mshindi wa pili, Nigeria, alipata zawadi ya dola milioni 4.
Katika michuano hiyo inayoendelea nchini Morocco, timu zitakazotoka katika hatua ya nusu fainali zitajinyakulia dola milioni 2.5 kila moja, huku zile zinazotinga robo fainali zikipokea dola milioni 1.3 kila moja.


0 Comments