MIL.900 KULETA MAJI SAFI SINONIK
LONGIDO: Fedha Sh milioni 90 zimechangwa ili kuvuta maji kutoka chanzo cha maji kilichopo kata ya Sinonik, Wilaya ya Longido kwa lengo la kuwahakikishia wananchi wa kata hiyo maji safi na salama.Kiasi hicho cha fedha kitawezesha pia mabomba, ujenzi wa tanki lita 100,000 na ujenzi eneo la maji ya mifugo.
-
Fedha hizo zimechangwa na Naibu Waziri wa Madini, Dk Steven Kiruswa, wananchi wa kata hiyo na shirika lisilo la kiserikali la Pingo's Forum.-Dk Kiruswa pekee alinunua mabomba ya maji ya Sh milioni 18, na wananchi milioni 2, ili kusambaza maji maeneo ya vijijini umbali wa km 4.
-
Akizungumza leo Desemba 25, Dk Kiruswa amesema chanzo hiko cha maji ni muhimu, hivyo aliwaomba wananchi kulinda miundombinu yake kwa gharama kubwa.
-Amesema chanzo hiko kilichopo mpakani mwa Kenya kilikuwa kikitumiwa na wananchi wa taifa hilo, baada ya kutandaza mabomba ya maji toka chanzo hicho, hali hiyo iliwafanya wananchi wa Sinonik kupata changamoto ya maji.

0 Comments