MATOLA 10 WALIOFANYA KAZI NA SELEMANI MATOLA

Simba wameanza mchakato wa kutafuta kocha mpya wa kuinoa timu hiyo baada ya kumchania mkataba aliyekua meneja wa timu hiyo Dimitriv Pantev.Kwa sasa kikosi cha timu hiyo kipo chini ya Kocha Msaidizi Selemani Matola ambaye amedumu na timu hiyo kwa muda mrefu katika nafasi hiyo. Kwa nyakati tofauti Matola amedumu kama Kocha Msaidizi akiwa amefanya kazi makocha 10 walioingia na kutoka na kumuacha katika nafasi hiyo.Ifuatayo ni orodha ya makocha wa waliofanya kazi na mzawa huyo. Patrick Aussems, Sven Vanderbroeck, Didier Gomes, Pablo Franco Martin, Zoran Mark, Juma Mgunda, Robertinho, Adelhaick Benchikha, Fadlu Davids, Dimitriv Pantev. Je ni wakati wa Simba kumuamini Matola kukiongoza kikosi cha timu hiyo kutokana na uzoefu alioupata kutoka kwa makocha mbalimbali wa kigeni?

Post a Comment

0 Comments