NAUONA MWISHO WA UFALME WA MO SALAH

Nauona mwisho wa ufalme wa Salah pale Liverpool,Salah ameisaidia Salah Liverpool kwenye mafanikio yao kwa miaka alokaa pale ila kwa hapa walipofikia ni rahisi kutabiri kuwa Mo Salah ataondoka Liverpool. Ni bora angekuwa majeruhi ila mzima wa afya ila gafla tu ameanza kuwekwa benchi kutokana na kiwango chake so sad. Mbaya zaidi kikosi kinachoenda Italia kwenye mchezo dhidi ya Inter wiki ijayo kocha Arne Slot amemuacha yaani hatokwenda kabisa bora ile ya kukaa benchi hii inamaana hata benchi hawamtaki. Kingine kibaya kuliko mashindano ya AFCON yamefika ataenda kuitumikia Misri sasa hapo ndiyo ukute timu inapata matokeo baaasi unaonekana wewe ndiyo tatizo kinachofuata ni kutemwa mazima. KING wa Misri anapitia kipindi kigumu sana nahisi hata yeye hajategemea.

Post a Comment

0 Comments