MASTAA watatu wa kimataifa wakiongozwa na mshambuliaji Andy Boyeli,kiungo Balla Conte na winga Celestine Ecua huenda wakatolewa kwa mkopo kutokana na viwango vyao kushindwa kulikuna benchi la Ufundi la timu hiyo.
Kocha Pedro Gonçalves amewaangalia nyota hao kupitia mechi kadhaa za Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwaagiza viongozi wa klabu hiyo kuwatoa kwa mkopo ili wakaimarishe viwango vyao huku nafasi zao akigiza waletwe mastaa wengine wakali.
Chanzo cha taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga,kimelieleza gazeti hili kwamba,benchi la Ufundi la timu hiyo limeanza operesheni ya kusafisha kikosi chake kwa kufanya mabadiliko muhimu ya wachezaji ambapo panga limeanza kuwapitia nyota hao kabla ya kwenda kwa wengine.
Boyeli huenda akarudishwa katika klabu yake ya zamani Sekhukhune FC ya Afrika Kusini wakati Balla Conte anaweza kupelekwa kwa mkopo Mbeya City FC na Ecua akipelekwa Singida Black Stars.Hatua hiyo inaonesha mwelekeo mpya wa Yanga katika kupanga kikosi chenye ushindani zaidi kwa msimu huu kabla ya dirisha kufunguliwa rasmi Januari mwakani.

0 Comments