Taka za bia zinavyotumika kutengeneza maziwa
Wataalamu na sekta ya bia wamegundua matumizi mapya yasiyo ya kawaida kwa mashudu ya shayiri – bidhaa kubwa inayozalishwa kama taka kutoka sekta ya bia.
Hata hivyo, kwa watumiaji wa kinywaji hicho ni nadra kufikiri kuhusu milima ya mashudu inayojikusanya kama taka kubwa zaidi ya baada ya kutengenezwa bia.Hii inajulikana kama mashudu ya shayiri. Karibu gramu 200 (7oz) huzalishwa katika kila lita moja ya bia inayotengenezwa.
Duniani, takriban tani milioni 37 za mashudu huzalishwa kila mwaka – sawa na uzito wa mabasi 340. Na tunapoongeza matumizi ya bia – mauzo yanatarajiwa kupanda kwa theluthi moja katika miaka saba ijayo – yatazalishwa zaidi.
Viwanda vikubwa vya bia vimeunda hata maziwa ya shayiri ya vegan yanayotokana na mashudu ya shayiri.Viwanda vikubwa vya bia vimetengeneza bidhaa nyingine kama maziwa ya shayiri yanayotokana na taka za shayiri.
Karibu 70% ya mashudu ya shayiri yanayotokana na biogas kwa sasa hutumika kama chakula cha mifugo, wakati 10% hutumika kutengeneza bayogesi huku karibu asilimia tano hutumwa moja kwa moja kwenye taka – jambo linaloongeza gharama kwa viwanda vya bia – ambapo huoza na kuzalisha gesi ya methane angani.
Lakini ndani ya bidhaa hii ya bia kuna kemikali nyingi muhimu ambazo zinaweza kutumika, ikiwa ni pamoja na protini nyingi.Watafiti na kampuni sasa wanatafiti juu ya namna gani kemikali hizi zinavyoweza kutumika kwa manufaa zaidi.
Kampuni ya Upgrain kutoka Uswisi ni mojawapo. Mwaka 2024, ilizindua mfumo wa kuchakata mashudu ya shayiri na kuyageuza kuwa protini na nyuzinyuzi, ambayo imethibitishwa kuwa salama kwa matumizi ya binadamu na taasisi ya Marekani ya Food and Drug Administration (FDA) na mamlaka ya usalama wa chakula ya Ulaya European Food Safety Authority (EFSA) (kwa sababu mashudu ya shayiri bado ni nafaka).
Brauerei Locher, mzalishaji wa bia wa pili kwa ukubwa nchini Uswisi, alizindua mnamo Septemba 2024 na sasa unajenga kituo kikubwa zaidi cha uchakataji wa mashudu ya shayiri barani Ulaya.
William Beiskjaer, mwanzilishi mwenza wa Upgrain, anasema kwamba mashudu ya shayiri ni "hazina iliyofichika katika suala la lishe endelevu na yenye afya."
Anasema inaweza kusaidia kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya kimataifa ya protini."Kuna ongezeko la uhitaji wa kuboresha chakula, hasa ili kuongeza protini na nyuzinyuzi kwenye mlo wetu," anasema.
Mashudu ya shayiri ni chanzo tajiri cha virutubishi ambavyo mara nyingi hutumika kama chakula cha mifugo na huzalisha methane inapoharibika kwenye taka.Mashudu haya hutengeneza bidhaa mbalimbali kama vegan, vyakula vya kuoka, crisps, na hata kahawa; pia ina uwezo wa kutumika katika shughuli za ujenzi, kutengeneza vipodozi na karatasi.
Si bidhaa zote zimepitia mchakato huu, baadhi ya bidhaa zinaweza kukutana na changamoto za kupokelewa na watumiaji.Vilevile, kuchakata mashudu ya shayiri kunahitaji nishati nyingi na huharibika haraka.
Hata hivyo, wataalamu na watengenezaji tayari wanashughulikia changamoto hizi.Viwanda vikubwa vya bia kama Anheuser-Busch InBev kutoka Ubelgiji na Molson Coors kutoka Chicago vimeunda bidhaa zao za maziwa ya shayiri ya vegan zinazotokana na mashudu ya shayiri. Molson Coors inadai kuwa bidhaa yake ya Golden Wing ina "ladha tajiri na yenye creami" na ina sukari 25% kidogo kuliko maziwa mengi ya shayiri.
"Hii ni wazo jipya la kusisimua," anasema Beiskjaer. "Kama ungeniambia miaka minne iliyopita kwamba mashudu ya shayiri ya waandaji bia yatakuwa chanzo cha chakula cha [binadamu], ningejiuliza unasema nini. Lakini sasa tuko njiani kuona BSG inayosindikwa kuwa bidhaa muhimu katika sekta ya chakula."
Beiskjaer anasema anaelewa kwa nini baadhi ya watu wanaweza kuwa na wasiwasi kuhusu dhana ya "chakula kilichosindikwa tena". "Lakini tunahitaji kueleza kwamba mashudu ya shayiri ya waandaji bia si bidhaa ya taka," anasema. "Inahifadhiwa ili isitumiwe kama taka."
Viwanda vikubwa vya bia kama Anheuser-Busch InBev kutoka Ubelgiji na Molson Coors kutoka Chicago vimezalisha bidhaa zao vegan zinazotokana na mashudu ya shayiri.
Molson Coors inadai kuwa bidhaa yake ya Golden Wing ina "ladha yenye mvuto" na sukari 25% kidogo kuliko maziwa mengi ya shayiri.
"Hii ni wazo jipya la kusisimua," anasema Beiskjaer. "Kama ungeniambia miaka minne iliyopita kwamba mashudu ya shayiri ya watengeneza bia yatakuwa chanzo cha chakula cha [binadamu], ningejiuliza unasema nini.
Lakini sasa tuko njiani kuona BSG inayosindikwa kuwa bidhaa muhimu katika sekta ya chakula."
Beiskjaer anasema anaelewa kwa nini baadhi ya watu wanaweza kuwa na wasiwasi kuhusu dhana ya "chakula kilichosindikwa tena". "Lakini tunahitaji kueleza kwamba mashudu ya shayiri yanayotokana na bia si bidhaa zinazotokana na taka," anasema. "Inahifadhiwa ili isitumiwe kama taka." BBC
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
0 Comments