KOCHA YANGA AKILI YOTE KWA AL AHLY



NA MWANDISHI WETU
KOCHA Mkuu wa Yanga,Pedro Gonçalves ameziangalia mechi za michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ambazo timu yake inakwenda kucheza mwakani na kusema akili yake inaipigia hesabu kali Al Ahly ya Misri ili kupata ushindi ugenini.
Al Ahly watakua wenyeji wa Yanga Januari 23 mwakani mchezo utakaopigwa uwanja wa Cairo International
kabla ya timu hizo kurudiana Januari 30 uwanja wa Amaan Complex mjini Zanzibar.
Pedro ameliambia gazeti hili kwamba,anatambua Al Ahly ni wagumu wakiwa nyumbani lakini mikakati yake ni kuondoka Cairo na alama tatu muhimu ili kujiweka sawa na mbio za kufuzu robo fainali ya michuano hiyo namba moja kwa utajiri ngazi ya klabu barani Afrika.
Alisema,kwenye mchezo wa soka lolote linawezekana licha ya kwamba watu wanaamini Yanga haiwezi kuvuna alama mbele ya Waarabu hao lakini tayari ameanza kuichomea kichwa Al Ahly ili kupata pointi kutoka mikononi mwao ili kuchonga vyema barabara ya kuandika historia mpya kwa klabu hiyo.
Aidha Kocha huyo alisema,licha ya kuumizwa kichwa na Al Ahly lakini kikosi chake hakiwezi kumdharau mpinzani yoyote kwenye kundi lao ambalo lina timu za JS Kabaylie na Far Rabat.
Pedro alisema,atatumia uzoefu wake wa kufundisha muda mrefu soka barani Afrika kuiletea Yanga mafanikio katika ngazi ya kimataifa na kutetea mataji yake yote ya ndani.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@


Post a Comment

0 Comments