"NEEMA" YA BIMA LEE ULIVYOGUSA MASHABIKI NA WATANGAZAJI

NA JIMMY CHIKA
(Tembo Mpweke)

BIMA Lee ilikuwa haishikiki wanamuziki walikuwa wamezoeana sawasawa.

Safu ya uimbaji iliyokuwa na Shaaban Dede, Jerry Nashon, Othman Momba, Roy Bashekanako na Jumbe Batamwanya ilitengeneza Combination kali ile mbaya.

Achilia mbali mapacha watatu wa magitaa Abdalah Gama, Joseph Mulenga na Suleyman Mwanyiro Bima Lee ilikuwa imetimia sawasawa.

Licha ya kupata wanamuziki hao wakali lakini Bima lee mpya ya mwaka 1984 ilipata utulivu wa hali ya juu baada ya kukaa kambini kwa muda mrefu.

Kambi hiyo iliyokuwa kigamboni ilitimia kila kitu malazi pia mpishi maalum aliyekuwa akibadilisha milo baada ya kushauriana na wanamuziki.

Hakukuwa na kazi nyingine ni muziki tu, tena kipindi hicho ilikuwa kama Suprise baada ya mpiga gitaa la solo mwingine kutia timu kambini akitarajiwa kuwa msaidizi wa Mulenga, huyo ni Michael Bilali aliyetokea pia Vijana jazz.

Hivyo Mulenga akamkabidhi gitaa mgeni huyo ili afanye yake katika wimbo wa Neema.

Waimbaji walionekana kuufurahia sana wimbo huo hasa Momba alionekana kutamani kutengeneza pande litakalofunika na kweli ikawa hivyo.

Dede yeye alicheza kama kiungo wa kati katika wimbo huo huku akiwaacha akina Jerry Nashon wakijiachia.

Hatimaye wimbo huo ukakamilika na siku hiyo ukawa unatambulishwa katika onyesho la mchana pale Mbwisi bar Manzese.

Ilikuwa balaa kubwa wanamuziki na mashabiki wote walionekana kuchabgamka kupita maekezo haikuwa rahisi kumuona mtu kitini hasa wakati wa kupigwa kibwagizo cha wimbo huo.

Ulikuwa ni wimbo bora kwao na uliowapagawusha lakini hata ulipotua katika studio za RTD kwa ajili ya kurekodiwa watangazaji waliupenda sana na kusababisha uwe unasikika kuanzia vipindi vya alfajiri hadi usiku.

Post a Comment

0 Comments