NA SANIA MOHSIN
UONGOZI wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara,Yanga umeuteua mchezo wao wao wa kesho dhidi ya Fountain Gate uwe maalumu kwa ajili kumpongeza kipa wao wa kimataifa Djugui Diara kutokana na kazi kubwa anayoifanya ndani ya kikosi cha timu hiyo.
Itakumbukwa Jumamosi iliyopita kule nchini Algeria ambako Yanga ilikuwa na mechi ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Kabylie, Diara aliibuka nyota wa mchezo kutokana na kuokoa nafasi nyingi za wazi ambazo ilikuwa timu hiyo ifungwe mabao.Lakini pia ni Diara huyo alikua ametoka kufanya kazi kubwa nyingine katika mchezo wa michuano dhidi AS Far Rabat ya Morocco kule uwanja Amaan Complex na kuiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu itapigwa Alhamis wiki kwenye uwanja wa KMC Complex,Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo itakuwa ni siku maalumu kwa mashabiki wa klabu hiyo kumtunza Diara kwa chochote walichonacho.
Kabla ya uongozi kuridhia wazo hilo kulikuwepo na shinikizo la mashabiki kutaka kupangwa kwa 'Diara maokoto Day'kama njia ya kumuonesha upendo kipa huyo kwa namna anavyoipigania Yanga katika michuano ya kimataifa na Ligi Kuu.
Afisa Habari wa Yanga,Ally Kamwe,amenukuliwa akisema,mechi dhidi ya Fountain Gate imetengwa maalum kwa ajili kipa huyo ambapo makapu yatazungushwa uwanjani ili kumtunza Diarra.Alifafanua kwamba wanachama wa Mikoani watume maokoto yao kwa wawakilishi wao waliopo hapa Dar es Salaa watakaokabidhi siku hiyo pale uwanjani.
.jpg)
0 Comments