DCEA yataifisha mali za wahalifu Dawa Kulevya zenye thamani ya shilingi bilioni 3.304.


 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amesema kuwa DCEA imetaifisha mali za wahalifu wa dawa za kulevya zenye thamani ya shilingi bilioni 3.304. Hatua hii imekuja sambamba na operesheni mbalimbali zilizowezesha kukamata jumla ya kilogramu 3,799.22 za dawa za kulevya, kuteketeza ekari 18 za mashamba ya bangi, pamoja na kuwakamata watuhumiwa 84 waliohusishwa na makosa hayo.


Ameeleza kuwa katika kuimarisha mapambano dhidi ya uhalifu wa dawa za kulevya, Mahakama Kuu – Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ilitoa amri ya kutaifishwa kwa mali hizo za watuhumiwa Saleh Khamis Basleman na Gawar Bachi Fakir, waliodaiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Mali zilizotaifishwa zinajumuisha nyumba, viwanja na magari.

Maamuzi hayo ya mahakama yalitokana na uchunguzi uliofanywa na DCEA, ambapo ilibainika kuwa mali hizo zilipatikana kupitia shughuli za uhalifu.

 Utaifishaji huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Mazao ya Uhalifu Sura ya 256, ikisomwa pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa Sura ya 200, pamoja na Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 ya mwaka husika.

Post a Comment

0 Comments