Na Ally Mandai
Rais wa Shirikisho la soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe, amethibitisha mipango ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), kuandaliwa kila baada ya miaka Minne.
Tangazo la ratiba mpya lilitolewa Jumamosi, Desemba 20 na kukomesha Utamaduni wa muda mrefu wa Mashindano hayo kufanyika kila baada ya Miaka miwili tangu 1968.
Mabadiliko ya muundo wa Mashindano hayo yataanza kutumika Michuano ya Mwaka 2027, ambayo Mashindano hayo yatafanyikia Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa Motsepe, mabadiliko hayo ni sehemu ya maono ya ujasiri kwa mustakabali wa soka la Afrika.
CAF pia imezindua Mipango ya Ligi ya Mataifa ya Afrika ambayo itaanza mwaka wa 2029.



0 Comments