CHAMA Cha Mapinduzi kimeeleza namna kitakavyoifungua Morogoro kwa ujenzi wa barabara ya lami itayounganisha mkoa huo na mkoa jirani wa Ruvuma.
CCM imewahakikishia wananchi kuwa katika Ilani yake ya Uchaguzi ya 2025-2030 itawafikia zaidi wakulima kwa kuendelea kutoa ruzuku ya mbolea na mbegu.
Wasira alieleza hayo kwa nyakati tofauti akizungumza na wana CCM na wananchi katika vikao vya ndani vya Chama na mikutano ya kampeni katika majinbo ya Malinyi na Ulanga, wilayani Malinyi, Mkoa wa Morogoro, jana.
"Tutafanya nini miaka mitano ijayo?, kwanza tutaendelea kuimarisha elimu maana elimu ndio msingi wa maendeleo na tunakusudia kujenga barabara ya kutoka Ifakara kuja Lupilo mpaka Malinyi, ipo katika Ilani na hiyo ni barabara moja tu.
"Tunajenga barabara inayounganisha Morogoro na Songea (mkoa wa Ruvuma) nayo itapita hapa hapa (Malinyi), wala siyo ndoto, makandarasi katika maeneo mengine wapo, tunataka kufungua eneo hili la Morogoro kwa sababu kwa muda mrefu limekuwa na miundombinu yenye matatizo," alisema.
Alisema katika ilani hiyo CCM imeielekeza serikali kusudi la kujenga madaraja mawili yanayosumbua katika barabara ya Ifakara-luoiro-Malinyi na Lupiro-Mahenge.
"Shabaha yetu ni kufungua eneo hili, eneo hili ni muhimu sana kwa uchumi, ndiyo, ninyi mnalima sana mpunga na lazima tuweke barabara mpunga ufike sokoni ili kazi yenu iwalipe kwa sababu mkifika sokoni bei ya mazao yenu itakuwa nzuri na ikiwa nzuri umaskini utapungua.
"Hizo ndizo ahadi za CCM, ahadi za ukweli na zinazotekelezeka, lakini bado tutajenga vituo sita vya afya katika eneo hili katika muda wa miaka mitano ijayo," alieleza.
Mbali na ahadi hiyo, alisema CCM itaielekeza serikali kuendelea kuimarisha miundombinu muhimu kwa ajili ya kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa mkoa huo na taifa kwa ujumla.
Katika ziara hiyo wasira alimwombea kura Mgombea urais kupitia CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan.

.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

0 Comments