MTANDAO WA BARABARA ZA LAMI HALMASHAURI YA KARAGWE KUFIKIA KM 28.9

Karagwe 

Wilaya ya Karagwe kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) imejikita kuongeza mtandao wa Barabara za lami kutoka kilometa 25.29 hadi kilometa 28.29  ifikapo  Novemba mwaka huu utakapokamilika mradi wa Barabara ya Nyakahanga ,_Nyabionza Masheli kilometa 3  za lami.

Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 imeweka jiwe la Msingi katika barabara hiyo ambayo Mradi wake umefikia asilimia 83

Meneja wa TARURA wilaya ya Karagwe  Mhandisi Kalembula Malimi amesema kuwa  serikali iliidhinisha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya matengenezo ya barabara hiyo kwa kiwango cha Lami na mpaka sasa mkandarasi amelipwa shilingi Bilioni 1.1  

Alisema barabara hiyo ni moja ya barabara zinazochochea uchumi wa wananchi  na kurahisisha huduma za jamii.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa Ndugu Ismail Ussi amewataka wananchi kutumia fursa za uwepo wa barabara kufanya biashara  kwa nyakati zote ili kukuza uchumi wao na kuchangia pato la Taifa,kupeleka watoto shule na kuinua familia zao.

Amesema Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara za vijijini kwani ndiko kwa wananchi wanaotegemea kusafirisha mazao kwa ajili ya kujipatia kipato na kuendesha familia zao kupitia barabara bora na imara .

Kwa Mujibu wa Meneja wa TARURA Wilaya ya Karagwe   kwa asilimia 78 barabara zake zinapitia muda wote huku asilimia 22 barabara zikiwa katika matengenezo na ukarabati wa Mara kwa mara.





Post a Comment

0 Comments