JAKAYA KIKWETE AWATAKA JIMBO LA KIVULE KUMCHAGUA OJAMBI MASABURI

 RAIS  Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete   amewataka wananchi wa Jimbo la Kivule Wilayani Ilala kumchagua Mgombea ubunge wa jimbo la Kivule Ojambi Didas Masaburi kwa nafasi ya Ubunge madiwani na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ili waweze kuleta maendeleo. 

Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alisema hayo jimbo la Kivule wakati wa  uzinduzi wa kampeni za jimbo hilo kumnadi mgombea ubunge Ojambi Masaburi na madiwani  sita.

"Wananchi wa Jimbo la Kivule nawaomba kura za Rais mpeni Dkt.Samia Suluhu Hassan za ubunge elekezeni kwa  Ojambi Didas Masaburi  ili aweze kuwaletea maendeleo ana sifa zote za kuwatumikia wananchi wa Kivule " alisema Kikwete.

Kikwete alisema maendeleo yanatokea sehemu zote kwa ajili ya Chama cha Mapinduzi wagombea wa CCM  ndio wenye kuleta maendeleo katika nchi yetu .

Kwa upande mwingine alisema Dkt.Samia ameimarisha  Mapato katika nchi yetu na kujenga mahusiano Kimataifa anapenda watu wake pia kwa kugusa maisha ya watu wote ikiwemo sekta ya afya kina Mama wanajifungua kwa uhakika vifo vya Mama na Mtoto kwa sasa hamna .

Kwa upande wake Mgombea ubunge Tarime Vijijini  Mwita Waitara, aliwataka wananchi wa Jimbo la Kivule na wenyeji wa Tarime wanaoishi jimbo la Kivule kumpigia kura Ojambi Masaburi anatosha pamoja na  Dkt.Samia Suluhu Hassan na madiwani wa Chama cha Mapinduzi ili waweze kuleta maendeleo. 

Mgombea ubunge jimbo hilo Ojambi Masaburi, alisema yeye anatosha kuwa Mbunge wa Kivule sababu amekaa katika Udiwani miaka kumi Naibu meya miaka nane Mwenyekiti wa Kamati za uchumi na huduma za jamii na vyeo mbalimbali hivyo uwezo wa kuongoza Jimbo hilo anaweza  na anatosha CV ya kuwa mbunge. 

Masaburi alisema wakati akiwa Naibu Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ameshirikiana na madiwani wa jiji hilo kuleta maendeleo Wilayani Ilala baadhi ya maendeleo ambayo ameweza kusimamia yaliofanywa na Serikali ya awamu ya sita ya Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya kata zote za Jimbo la Kivule vimejengwa vituo vya afya. 

Akizungumzia sekta ya maji Dkt.Samia amefunga tanki kubwa la maji Bangulo la Shilingi Bilioni 9 mtandao wa maji umewekwa kwa ajili ya kusambaza maji jimbo kivule.

Akizungumzia miundombinu ya Barabara kwa sasa ujenzi wa barabara Kitunda Kivule kwenda  Msongola umeanza kwa kiwango cha lami. 

Akizungumza barabara  zingine zinazojengwa kwa kiwango cha lami Pugu Majohe Viwege,Nyangaza Majohe Moshi Bar ,Machimbo Matembele,shule ya Misitu ,Hospitali ya Wilaya kivule,Picha ya Ndege Kanisa la Roma .

Mgombea ubunge jimbo la Ilala Mussa Zungu amemwagiza Mgombea ubunge Ojambi Masaburi akishinda nafasi yake ya Ubunge ashuke chini kwa wananchi kutatua kero aanze na mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri pamoja na sekta ya afya.








Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form