MAVUNDE AENDELEA NA KAMPENI KATA YA MAKOLE-JIMBO LA MTUMBA

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtumba kwa tiketi ya CCM Ndg. Anthony Mavunde ameendelea na awamu ya kwanza ya kampeni yake ya mtaa kwa mtaa kwa kila kata kuzungumza na makundi mbali katika maeneo husika.

Ndugu Mavunde leo alikuwa kata ya Makole na kutembelea na kuzungumza na wananchi wa Mitaa ya Makole NHC,Chadulu, na Chimuli ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwaombea kura Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. Samia S. Hassan na Mgombea Udiwani wa kata ya Makole Ndg. Omary Haji.











Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form