BABLEVO:CHAMA KITALETA MAKAMU WA RAIS MWINGINE

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Clayton Chipando ‘Baba Levo’, amesema anaamini Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina uwezo wa kumpata mtu mwingine wa kushika nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Dkt. Emmanuel Nchimbi kujiuzulu nafasi hiyo.

SOMA PIA,KATIBA:RAIS SAMIA ANA SIKU 14 ZA KUTEUA MAKAMU MPYA  

Baba Levo ametoa kauli hiyo leo, Agosti 26, 2026, baada ya kuwasili Bungeni na kuulizwa kuhusu uamuzi wa Dkt. Nchimbi kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais.

Akizungumza na waandishi wa habari, Baba Levo amesema CCM ni chama kikubwa chenye watu wengi wenye uwezo, hivyo anaamini kitapendekeza mtu mwingine ambaye ataendelea na majukumu hayo.

“Chama kitatoa kitu, Chama ni kikubwa sana na kina Watu wa kila aina, kwa hiyo Chama kitaleta kitu kipya, kitaleta Mtu mpya na tutasonga naye,” amesema Baba Levo.

Ameongeza kuwa kwa sasa wao kama viongozi na wanachama wa chama hicho wanaendelea kusubiri na kufuata maamuzi yatakayotolewa na chama, akisisitiza kuwa wao ni wadogo ndani ya chama na jukumu lao ni kusikiliza maelekezo ya chama.

Post a Comment

0 Comments